2 Chronicles 7:8-10

8 aHivyo Sulemani akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. 9 bKatika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi. 10Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Sulemani akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi Bwana Mwenyezi Mungu aliomtendea Daudi na Sulemani na kwa ajili ya watu wake Israeli.

Bwana Mwenyezi Mungu Amtokea Sulemani

(1 Wafalme 9:1-9)

Copyright information for SwhKC